Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ameonya dhidi ya uvamizi wa mashamba. Akizungumza hapo jana Jumapili Ramaphosa amesema hakuna mtu aliye na haki ya kuvamia ardhi na kukiuka haki za watu wengine. Chama cha African National Congress kimeanza kuchukua hatua kubadilisha katiba ili kiweze kuwapokonya watu mali pasipo kulipa fidia. Hatua hiyo ya chama cha ANC imeibua wasiwasi kua huenda mashamba yanayomilikiwa na wazungu yakavamiwa. Hata hivyo Ramaphosa amesema upokonyaji huo wa ardhi utafanyika kisheria na katika hali ambayo haitatishia uchumi na usalama wa chakula.

Maoni

Machapisho Maarufu