Mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam na maeneo ya jirani nchini Tanzania zimeleta athari na kadhia kwa baadhi ya watu, baada ya eneo la Jangwani barabara ya Morogoro kufurika maji na kusababisha ofisi za shirika la usafiri Dar es Salaam kusitisha safari zake kwa abiria. Pichani ni baadhi ya wakazi wakihangaika kupita eneo hilo lililofurika maji kuwahi katika shughuli zao. Tueleze eneo ulipo hali ikoje? Picha na Said Khamis.

Maoni

Machapisho Maarufu