Rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe amesema kwamba aliondolewa madarakani kwa kile alichokiita mapinduzi ya kijeshi. Mugabe aliyasema hayo katika mahojiano yake ya kwanza ya televisheni tokea aondoke madarakani mwezi Novemba. Akizungumza na na Shirika la utangazaji la Afrika Kusini, SABC, Mugabe mwenye umri wa miaka 94, alisema aliondolewa madarakani kwa nguvu na jeshi. Mugabe amesisitiza kuwa yalikuwa ni mapinduzi ya kijeshi na kusema wanapaswa kuiondoa aibu hiyo waliojiwekea wenyewe na kwamba hawaistahili. Tokea Mugabe kujiuzulu, mshirika wake wa zamani Emmerson Mnangagwa ameapishwa kama rais wa mpito.

Maoni

Machapisho Maarufu