Serikali ya Ufilipino imesema kuwa imeufahamisha rasmi Umoja wa Mataifa kwamba itajitoa katika mkataba ulioanzisha mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC, inayochunguza vita vya rais Rodrigo Durtete dhidi ya madawa ya kulevya. Hatua hiyo imekuja siku mbili baada ya Durtete kutangaza kuwa nchi yake ingejitoa katika mahakama hiyo kutokana na uchunguzi wake wa awali katika madai kwamba kampeni yake dhidi ya madawa ya kulevya ni uhalifu dhidi ya ubinadamu. Polisi nchini humo imesema wameua takribani washukiwa 4,000 waliopambana nao wakati wa kukamatwa. Lakini mashirika ya haki za binadamu yanadai kuwa idadi halisi ni mara tatu zaidi na wanaituhumu serikali kwa mauaji.

Maoni

Machapisho Maarufu